KUITAMBULISHA AMAwuli
AMAwuli Shule ya Sababu ni shule binafsi ya mtindo wa twisheni, ya jinsia zote, itoayo elimu kwa watoto kuanzia umri wa miaka tano (5) mpaka miaka nane (8). Ni tumaini letu kwamba mchakato wa elimu bora humwandaa mwanafunzi kwa ajili ya kujitegemea kama mtu mwenye mwelekeo na kusudi, na kwa mtoto katika shule ya AMAwuli, hili linalenga matakwa ya ukubwani. Mtaala wa elimu utolewao na AMAwuli umebuniwa ili kumkuza mtoto anayefikiria kwa kujichunguza, ambaye ameshikamana na hali ya umuhimu na kupewa uwezo wa kuishi maisha yenye mwelekeo wa suluhisho. Watoto hujifunza kuchukua umiliki na fahari katika kutafuta misingi ya ukuaji, uwepo, kukubali changamoto, kujifunza kutokana na vikwazo pamoja na kutafuta au kutengeneza fursa za kuendelea na kuwa bora! Kwa maana hiyo, kwa familia yenye kutaka malengo hayo, uamuzi wa wapi mtoto apate maandalizi yake kukabiliana na utu uzima, lazima utolewe kwa mawazo makini, uthubutu wa kutosha na kujitolea kunakoeleweka.
MASOMO:
MUHTASARI na MWONGOZO
Elimu katika AMAwuli Shule ya Sababu (AMASS) hujenga umahiri unaozingatia suluhu uliomiminwa katika kanuni za msingi za tabia, ambazo ni, Heshima, Kujali na Jukumu. Wanaosoma AMASS huvutwa kuelekea katika kujitambua na kujiongoza, ambapo wanafunzi hunufaika na stadi muhimu katika ujengaji hoja, ufahamu na suluhu. Kwa kupitia mazingira ya kutoa na kuhusisha, elimu ya AMASS ni mahsusi katika malengo yake ya jumla- kuwandaa wanafunzi kuwa wachukua hatua na watatuzi wa matatizo pamoja na wenye kujitambua thabiti na shauku ya kudumu ya kutafuta elimu zaidi ya ile ambayo tayari wanayo.
MALENGO na MAONO
AMAwuli Shule ya Sababu hukuza akili zenye uelewa zilizojengewa kanuni katika maadili yenye msingi wa kiutu. Kwa misingi hiyo, hili hufanyika pasipo mkanganyiko katika dhana, watoto siyo tu mstakabali, bali zaidi, mustakabali ambao wameandaliwa kuubeba kiwakili. Kwahiyo, huku wakielimishwa katika mazingira haya na kuongozwa kwa kanuni za Heshima, Kujali na Jukumu, vizazi vya watoto hawa vitaendelea huku vikiwa na mwelekeo; vikihudumu kama agano la thamani ya elimu; kuwa na uhusiano na umuhimu; kutoa mchango chanya kwa jamii na kupata ukamilisho katika uzoefu wa mwanadamu kwa ajili yao na wengine.
UJUMBE KUTOKA KWA MWANGALIZI MKUU
Wapendwa familia na marafiki,
AMAwuli Shule ya Sababu (AMASS) inabaki kuwa ya kweli katika kutoa elimu ambayo hukuza wateule katika njia ya kukuza umahiri wenye utafutaji wa elimu binafsi unaotambulika, ambapo kufikiri, kuelewa na uchukuaji hatua unaozingatia suluhisho katika mambo mbalimbali ni vya muhimu katika kuishi maisha makamilifu. Katika mazingira ya kujali na yenye nidhamu ya hali ya juu, tunahusiana katika itikadi iliyo hai ya UBUNTU - mshikamano wetu kama watu unaoangaliwa, ambapo "MIMI NI" kwa sababu "WEWE NI" na wewe ni kwa sababu "SISI NI!" Kwahiyo, MIMI pamoja na WEWE na SISI inakuwa SISI ambapo umuhimu wa mtu mmoja hutafsiriwa kama mmoja aliyefungwa kabisa katika kutambua na kukabili tatizo linalowaathili wamoja kwa kujituma.
Umakini wa hali ya juu katika kufuata maelekezo, mchakato na mawasiliano kati ya pande zote huwezesha maendeleo na udumishaji wa uaminifu na tabia sahihiza hulka. Mambo haya hutakiwa na wale walioaminishwa kuelimisha na kulinda afya za utu, kuanzia nafsi. Kati ya shule, nyumbani na jamii kwa jumla, tunazingatia katika uelewa wa kimabara wa ulimwengu, ambapo mmoja ni sehemu ya kitu kizima kilichounganishwa.
Tunaamini kwamba utafuata nidhamu na mtazamo ambao unapelekea wajibu kwa ajili ya kukua na mafanikio ndani na nje ya AMAwuli Shule ya Sababu..
Katika mshikamano na yaliyo ya msingi,
Dr. A.K. Tosu, f.SHr.
Mwangalizi Mkuu
Mkurugenzi Mkuu
SALAMU WAZAZI!!
Umuhimu wa kusudi, kujitolea katika kazi na kujali vipengele ni kiini cha mambo yanayofuatwa na AMASS. Mbele ya miaka yote tukiwa pamoja, tunaamini kwamba, pamoja na kujitambua kwa usimamizi na jukumu kama wazazi, wazee, waelimishaji na fanikio letu la pamoja kama miongozo, tutaangazwa kupitia uzoefu waliouishi watoto wetu kuelekea ukubwani. Asanteni sana kwa kujitolea kwenu kwa kuwa wenye nia katika kuchangia kuitengeneza sasa na baadaye.
Kama mzazi ambaye ana watoto wenye hali ya uhai hapa AMAwuli Shule ya Sababu utalifikia Jukwa la Wazazi. Hii itakuwa ndiyo njia yako kuu ya kujipatia taariza za jumla na mahsusi, ikiwa ni pamoja na udhibiti wa masuala yahusuyo mtoto. Sambamba na kutoa madokezo na kujibu maswali, kutakuwa na maelekezo ya mara kwa mara juu ya jukwaa hili ili kusaidia katika kupata matumizi mazuri ya rasilimali katika kila mwaka wa shule.
Pia utapata nafasi ya kuratibu mikutano ya uso kwa uso na vitivo, wafanyakazi na wakuu wa idara kadri itakavyohitajajika.
Tuna msisimko kuhusu kila mwaka wa shule na tunategemea kufanya mambo yaende pamoja!
Wenu,
Wasimamizi
TAARIFA
Unaomba taarifa za jumla kabla ya maombi? Tafadhali chagua ngazi unayotaka kuomba taarifa.
Umri wa Miaka 5-6
Umri wa Miaka 7-8
Quick Links
About
Admissions
Privacy Note